Afisa Kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Emmanuel Sungi leo Tarehe 28/08/2025 ameongoza kikao cha mafunzo kwa ajili ya maafisa ugani(kilimo) wapya ambao ni ajira mpya.
Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi mdogo wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu na kuhudhuriwa na maafisa ugani 15 kutoka katika kata.

Akitoa ufafanuzi Sungi amesema lengo la kikao hicho ni kutoa maelekezo namna ya kusajili wakulima kwenye daftari la ruzuku ya mbolea na mbegu,uwajibikaji na kufanya kazi kama timu moja na kupima afya ya udongo kwa wakulima zoezi ambalo wanatakiwa kuanza nalo mara moja.Pia wamepewa mafunzo ya namna ya kutumia mfumo wa ESS.

“Mkawajibike na kutenda haki kwa watu wote,fateni sheria na miongozo inavyotaka,nyinyi ni maafisa ugani na sio maafisa ardhi hivyo migogoro ya mipaka ya ardhi na mashamba haiwahusu”.Alisema Sungi

Naye Afisa Kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Obeid Sabori aliwataka maafisa ugani wote wakiwa na changamoto kwenye kata zao wasisite kuziwasilisha kwao ili kuweza kuzitatua kwa pamoja na kujengeana uwezo.
Mwisho maafisa ugani walipewa elimu kuhusu ufanyaji wa tathmini ya mazao na kukabidhiwa madaftari ya kusajili wakulima kwa ajili ya ruzuku ya mbolea na mbegu.

Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.